• +255 753 461 725

Huduma Zetu

Onfon Media Tanzania limited ni kampuni inayojishughulisha na kutoa huduma za ziada za simu ya Kiganjani ,kwa kushirikiana na mitandao mbalimbali ya simu nchini Tanzania. Tunaelewa mahitaji yako wewe mteja wetu mpendwa na tumejipanga kukupa kile utakacho kupitia huduma zetu zilizoandaliwa na watu mahiri na wenye ubunifu mkubwa. Huduma tunazotoa ni miito maalumu ya simu kwa wakupigiao ,meseji murua za kimahaba ,taarifa motomoto za soka la ndani na nje ya nchi , mafundisho ya biblia /qur'ani tukufu kwa kupitia ujumbe mfupi wa SMS.

MIITO KWA WAKUPIGIAO

Huduma hii ni kwa ajili ya kuwaburudisha ndugu,jamaa na marafiki kila wanapokupigia. Huduma hii inakupa fursa ya kuwafurahisha wakupigiao kupitia miito mbalimbali ya aina yake ikiwemo miito spesho kwa wapendwa,muito wa jina lako,Amri za Mungu,sala mbali mbali (kama baba yetu,Neema,Atukuzwe na kadhalika).

JINSI YA KUTUMIA HUDUMA

Kuna namna mbalimbali za kujiunga na kufurahia huduma zetu za miito kwa wakupigiao.
a. VODACOM
1. Miito spesho misimu mbali mbali ya sikukuu
Faida za Huduma hii
Inasaidia kuwashirikisha wanaokupigia kwenye shamrashamra za sikukuu mbalimbali kila wanapokupigia kwenye misimu/sikukuu husika. Piga *149*01*61# kisha chagua 1 kisha chagua sikukuu husika(mfano krismasi,mwaka mpya,pasaka,siku ya mtoto wa Afrika,Siku ya wanawake Duniani,Maulidi,Mwezi Mtukufu wa Ramadhani,Siku ya Uhuru).
Miito spesho misimu mbali mbali ya sikukuu
Hudama hii inasaidia kuwashirikisha wanaokupigia kwenye shamrashamra za sikukuu na misimu mbalimbali ya sikukuu husika.
Kujiunga
Piga *149*01*61# kisha chagua 1 kisha chagua muito wa sikukuu unayoitaka mfano:Krismasi,Mwaka Mpya, Uzalendo,Siku ya wapendanao n.k.
2. Miito spesho kwa wapendwa wako
Inakuwezesha kumzawadia mpendwa wako muito maalum kwa ajili yake unaosikilizwa na yeye tu kila wakati anapokupigia, hivyo anajihisi kupendwa kwa kweli na wewe unayempigia simu.Ijribu sasa! Piga *149*01*61# kisha chagua lugha > 1 > 5(Muito spesho kwa wapendwa wako).
3. Miito ya Jina lako
Huduma hii inawawezesha wanaokupigia kuthibitisha na kuwa na uhakika kwamba kwa kweli wewe ni mhusika ambaye wamelenga kumpigia Kupata huduma hii,piga sasa *149*01*61# kisha chagua 2 (Jina lako kama muito).
4. Miito ya maana ya Jina lako
Faida za Huduma hii
Inasaidia wanaokupigia kufahamu maana halisi ya jina lako kila wakupigiapo kama jina lako. Kupata huduma hii, piga sasa *149*01*61# kisha chagua 6 (Maana ya Jina Lako).
5. Miito ya Sala na Amri 10 za Mungu
Faida za Huduma hii
Huduma hiiinasaidia kuwakumbusha wanaokupigia sala muhimu pamoja na amri kumi za Mungu hivyo inawakuza kiroho Kupata huduma hii,Piga sasa *149*01*61# chagua 1 kisha 6 (Miito ya sala & Amri 10 za Mungu).
Jinsi ya Kusitisha Huduma
Kusitisha huduma ya miito kwenye mtandao wa Vodacom, mtumiaji anapaswa kupiga *149*01*61#, chagua 7 (Matumizi ya Huduma), kisha 3 (kufuta muito) Chagua usajili wako usioutaka (aidha 1, 2, 3 n.k) Hivyo, usajili wako usioutaka utasitishwa.
b. TIGO
1. Miito ya maana ya Jina lako
Piga *147*00*6# kisha chagua 7 (Name Tune).

HUDUMA ZA SMS

a. SMS ZA KIMAHABA
Huduma hii inakupa wewe mteja wetu mistari mitamu ya kimahaba kwa ajili ya yule umpendaye. Kupata huduma hii,tuma neno PENZI kuenda 15630 na unogeshe mahusiano yako leo. Mitandao husika ni Vodacom,Tigo & Airtel Huduma hii inakupa mistari murwa ya mapenzi na kukufanya uweze kunogesha na kustawisha mahusiano yako. Kujiunga: Tuma neno PENZI kwenda 15630. Huduma hii ni kwa mtandao wa Vodacom,Tigo & Airtel Pekee.
b. SMS ZA KABUMBU
Huuma hii itakupa taarifa motomoto za soka la ndani na nje ya nchi pindi zitakapo tufikia.
Kujiunga
Tuma neno SOKA kwenda 15630 na uhabarike kisoka.Hii ni kwa mitandao ya Vodacom,Tigo na Airtel.
c. SMS ZA MISTARI YA BIBLIA NA MAFUNDISHO YA KIKRISTO
Huduma hii inakupa wewe mteja wetu mistari ya maandiko takatifu kukufariji na kukuimarisha kiroho. Kupata huduma hii,tuma neno INJILI kuenda 15640.Hii ni kwa mitandao ya Vodacom,Tigo na Airtel.
d. SMS ZA MISTARI YA QUR'ANI TUKUFU NA MAFUNDISHO YA KIISLAMU
Huduma hii inakupa mistari ya maandiko Qur'ani tukufu na mafundisho ya kiislamu kwa ujumla Kupata huduma hii,tuma neno KURAN kuenda 15640.Hii ni kwa mitandao ya Vodacom,Tigo na Airtel.

VIGEZO NA MASHARTI

- Ujumbe wa kumtarifu mteja kuwa amefanikiwa kujunganisha au kusitishwa kwenye huduma itatolewa BURE.
- Ujumbe wa Huduma utatumwa kila siku kwa wateja pekee waliofanikiwa kutozwa gharama za huduma.
- Iwapo mteja hatofanikiwa kulipia huduma kwa siku 60 mfululizo, mfumo utasitisha usajili wa huduma.
- Kujiondoa kwenye huduma,tuma neno ONDOA (Jina la huduma) kwenda kwa namba uliyounganishwa nayo kwenye huduma,mfano ONDOA KURAN kwenda 15640.